tangazo 1

Tangaza Biashara Yako Kwa Gharama Nafuu -Tangaza Na Maisha Kiasi...!BLOGU LEO!!

Tangaza Biashara yako hapa kwa bei nafuu wasilana nasi kupitia +255 656 704 111 au +255 717 070 120 wote mnakaribishwa.

Monday, May 20, 2013

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AHANI MSIBA WA MZEE ALLY SYKES JIJINI DAR LEO



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitia saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa marehemu Ally Sykes, wakati alipofika kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiaga na baadhi ya wazee waliohudhuria shughuli za msiba, wakati alipokuwa akiondoka baada ya kuhani msiba wa mwasisi wa TANU, Ally Sykes, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anatarajiwa kuzikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimfariji mjane wa marehemu Ally Sykes, Zainab Ally, wakati alipofika kuhani msiba huo wa mwasisi wa TANU, aliyefariki jana jijini Nairobi. Marehemu Sykes anazikwa leo jioni jijini Dar es Salaam.

MATUKIO BUNGENI WAKATI WA UWASILISHAJI WA BAJETI YA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

IMG_1416Mbunge wa Mafia  Mhe. Abdulkarim Shah akiuliza swali la nyongeza bungeni IMG_1438Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika Mhe.  Adam Malima, akizungumza na Waziri Mkuu mstaafu Mhe. Edward Lowassa ndani ya ukumbi wa Bunge leo. IMG_1451Mbunge wa Ubungo Mhe.John Mnyika akizungumza na mbunge wa Mbeya mjini Mhe. Joseph Mbilinyi ndani ya ukumbi wa Bunge leo. IMG_1475Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.  Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na Naibu wake Mhe. Amos Makalla bungeni kabla ya kusomwa kwa bajeti ya Wizara hiyo. IMG_1500 
Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Dk Fenella Mukangara akiwasilisha hoja bungeni leo
NA ZAWADI MSALLA-MAELEZO DODODMA.

ULINZI WAENDELEA KUWA MKALI MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI MFAWIDHI WILAYA YA IRINGA JIONI HII......LIVE

 Askari  wa FFU  wakiendelea  kulinda  eneo la mahakama ya  wilaya ya Iringa  jioni ya leo  huku watuhumiwa  wakiwa bado kutoka mahakamani
 
 Ulinzi  mkali kweli kweli
 
 Karani  wa mahakama  Bi , Grace  akiita majina ya  wadhamini mahakamani hapo
 Pamoja na kesi hiyo  kuvuta  watu  wengi bado shughuli za mahakama  ziliendelea kama kawaida  pichani na hakimu  wa mahakama ya mwanzo bomani Mh. Alois Masua  akiendelea  kuwajibika kwa  wengine
 Wakuu  wa  FFU mkoa  wa Iringa  wakiwa kikazi zaidi nje ya mahakama hiyo  jioni ya leo katikati ni mkuu  wa FFU Bw Said Abdalah  Mnunka ambae amesababisha amani  na utulivu katika mji  wa Iringa

MBUNGE MSIGWA NA WENZAKE WAACHIWA KWA DHAMANA 27 WAKOSA DHAMANA KESI KUTAJWA TENA 3 MWEZI WA 6


 
Mbunge  Msigwa akishuka katika gari ya  polisi huku akiwa chini ya ulinzi mkali  wa  FFU leo  alipofikishwa mahakamani kabla ya  kudhaminiwa

 Mheshimiwa mbunge  Msigwa  akishuka katika gari ya  polisi chini ya ulinzi mkali  wa polisi
 Mkuu  wa FFU Iringa Said Abdalah Mnunka  (katikati) akiwa na maofisa  wenzake  wa  polisi
 Katibu  wa Chadema wilaya ya Iringa mjini Bi Suzana Mgonakulia  akitoa nje ya mahakama hiyo

 



 mbunge Msigwa akiwa amebebwa  juu juu na  wafuasi  wa Chadema jioni  hii

SAKATA la vurugu  za machinga na polisi mjini Iringa limechukua  sura  mpya  baada  ya  jeshi la  polisi mkoa wa Iringa  kumfikisha mahakamani mbunge  wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa pamoja na  watuhumiwa wengine zaidi ya 70

Huku mahakama   hiyo  ikitoa masharti nafuu ya dhamana kwa  watuhumiwa hao na  kuwaonya  kutofanya  kosa kwa  kipindi  chote  cha kesi  hiyo inapoendelea  kusikilizwa .

Watuhumiwa hao  walifikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wa wilaya ya Iringa Mheshimiwa Godfrey Isaya  leo  majira ya saa 8 mchana  huku wakiwa  chini ya ulinzi mkali  wa askari  wa kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa na msafara  wa magari zaidi ya matatu  likiwemo  gari ya maji ya  kuwasha .

Mbali ya mbunge Msigwa  kupanda gari ndogo  ya  wazi ya  polisi pamoja na  watuhumiwa  wawili wanawake  waliokamatwa katika  vurugu  hizo bado  watuhumiwa  wengine zaidi ya 70  walitumia usafiri wa karandinga la polisi .

 Mbele  ya mahakama  hiyo  wakili  wa serikali  Adolph Maganda alisema  kuwa  watuhumiwa hao kwa pamoja  wanatuhumiwa  kwa kosa kwa makosa matatu  likiwemo la kufanya kushiriki  mkutano na kufanya   vurugu ,uchechezi na kuharibu mali kinyume na sheria 

 

Huku mbunge  akisomewa mashitaka mawili likiwemo  kushawishi   na kufanya mkutano bila  kibali  .
Watuhumiwa  wote  wamekana  mashitaka  dhidi yao  huku  wakili  wa  serikali akidai  kuwa hana pingamizi na dhamana kwa  watuhumiwa hao wote  hata  hivyo wote   wamekana  mashitaka  yote yaliyotolewa  dhidi  yao .

Hata  hivyo makimu anayesikiliza kesi  hiyo alisema kuwa dhamana kwa  washitakiwa  wote  ipo  wazi  kwa kila mmoja kuwa mdhamini mmoja anayeaminika pamoja na kusaini hati ya dhamana  ya Tsh milioni moja .

 Hadi majira ya  saa 10 jioni mahakama  hiyo  ilikuwa ikiendelea na mchakato  wa  kupitia barua  za dhamana kwa  wadhamini  huku  mbunge akiwa  wa kwanza kudhaminiwa ,mbali ya  mbunge  watuhumiwa kati ya 74  waliokuwa  bado kupata  wadhamnini  ni  watuhumiwa  sita pekee.

 Katibu  wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) wilaya ya Iringa mjini Suzana Mgonakulima alisema  kuwa  mchakato  wa  kuwadhamini  watuhumiwa  wote  waliosalia unaendelea kufanyika na kuwa wana uhakika wa  watuhumiwa  wote kudhaminiwa .

Hadi  majira  haya  ya saa 10 .40  mbunge  msigwa na  wengine  wameachiwa  huku  watuhumiwa 27 kati ya 74  wamekosa  dhamana hadi kesi hiyo itakapotajwa  tena tarehe 3 /6/2012  
Wakati  huo  huo  wananachi  waliofika  mahakamani hapo  kushuhudia mbunge  wao akifikishwa mahakamani  wamempongeza mkuu  wa  kikosi cha kutuliza ghasia mkoa  wa Iringa (FFU) Said Abdulah Mnunka  kwa kusimamia amani na utulivu katika  eneo hilo la mahakama na jinsi ambavyo alivyoweza  kupambana na machinga  pasipo kumwaga damu kwa  siku ya  jana wakati  wa vurugu  hizo. KWA HISANI YA FRANCIS GODWIN BLOG

JK,MWINYI, MKAPA, BILAL WAMZIKA SYKES

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Rais wastaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kianana wakiungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Mzee Ally Kleist Sykes, mmoja wa waasisi wa chama cha TANU, jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. (PICHA NA IKULU)

Saturday, May 18, 2013

Dk Shein akutana na balozi wa Indonesia jana


 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania  na Rais leo asubuhi
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Balozi wa Indonesia nchini Tanzania Mhe Zakaria Anshar,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akimsindikiza mgeni wake Balozi wa Indonesia nchini Tanzania  Mhe Zakaria Anshar,alipofika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi baada ya mazungumzo yao. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu, Zanzibar

TAHARIFA YA IKULU JUU YA PROF.IBRAHIM LIPUMBA

KAULI ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa 
Ibrahim Lipumba, kwamba kuna njama za kumwongezea
 Rais Jakaya Kikwete, muda wa kuongoza nchi, ni uzushi 
mtupu na ni upotoshaji usiokuwa na msingi.
Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu iliyotumwa 
kwa vyombo vya habari juzi, ilifafanua kwamba Rais Kikwete
 hafahamu kuwepo mipango hiyo, na kumtaka Profesa 
Lipumba aisaidie jamii kusema nani anafanya mpango huo,
 ili ukweli ujulikane.
“Aidha, Mheshimiwa Rais anawasihi wanasiasa na Watanzania 
kwa ujumla, kuacha tabia za uongo na uzushi na kuwapotezea 
muda Watanzania kufikiria mambo yasiyokuwepo.
“Ukweli ni kwamba, kama ambavyo amesema mara nyingi,
 ni matarajio ya Rais Kikwete kuwa mchakato wa Katiba utakamilika 
mwaka 2014, na kuwezesha Uchaguzi Mkuu wa 2015 kufanyika chini 
ya Katiba Mpya kama inavyotarajiwa ,” ilieleza taarifa hiyo.
Kwa mujibu wa Ikulu, Rais Kikwete anatarajia baada ya uchaguzi 
wa 2015, atapata nafasi ya kustaafu mwisho wa kipindi chake 
cha uongozi kwa taifa letu.

'Mtoto wa Mkulima' na Wabunge wa Iringa na Mbeya

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge kutoka mikoa ya Mbeya na Iringa kwenye makazi yake Mjini Dodoma Mei 16,2013. Kutoka (Kushoto) ni Mbunge wa Viti Maalum, Mary Mwanjelwa, Mbunge wa Viti Maalum Ritta Kabati, Mbunge wa Kalenga na Waziri wa Fedha, William Mgimwa, na Mbunge wa Mbozi, Godfrey Zambi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

LOWASSA AZINDUA KITABU CHA MTIKISIKO WA UCHUMI

 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (kushoto), akizindua kitabu kipya kinachoelezea mtikisiko wa uchumi karne ya 2000 na kuendelea, kiitwacho 'The Economic Crisis of the 2000s and Beyond', Dar es Salaam LEO. Katikati ni Mtunzi wa kitabu hicho Dk. Prosper Ngowi na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni iliyochapisha kitabu hicho ya Matokeo Publishers &Printers, Rosemary Sokile
 Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa (katikati), akizindua kitabu kipya kinachoelezea mtikisiko wa uchumi karne ya 2000 na kuendelea, kiitwacho 'The Economic Crisis of the 2000s and Beyond', Dar es Salaam leo. Kulia ni Mtunzi wa kitabu hicho Dk. Prosper Ngowi na Mchapishaji, Dk. Charles Sokile.
 Baadhi ya wadau waloshiriki kwenye uzinduzi huo
Dk. Ngowi akisaini moja ya vitabu vilivyonunuliwa leo. (PICHA ZOTE NA KAMANDA MWAIKENDA)

RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE ATEMBELEA KIWANDA CHA EAST COASTS OILS AND FATS KAMPUNI TANZU YA METL IKIWA NI KAMPENI YA KUHAMASISHA LISHE BORA NCHINI.

Afisa Mwajiri wa kampuni ya East Coasts Oils and Fats ambayo ni Kampuni tanzu ya MeTL Bw. Eric Buberwa akisalimana na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kuwasili katika kampuni hiyo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea kusalimiana na wadau mbalimbali wa masuala ya Lishe.
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb), akiteta jambo na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wakielekea sehemu ya kiwanda cha East Coasts Oils and Fats. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL Bw. Vijay Raghavan akifafanua jambo kwa Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kabla ya kukumimina Virutubishi vya Vitamini A katika Kinu cha kuzalisha mafuta kiwandani hapo ikiwa ni ishara ya kuhamasisha Lishe bora kwa walaji.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimimina mafuta ya virutubishi katika kinu cha kutengeneza mafuta ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kampeni ya kuhamaisha Lishe bora kwa walaji kwa kuongezaji Virutubishi vya Vitamini A katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani, wakati alipotembelea Kiwanda cha EAST COAST OILS & FATS ambacho ni kampuni tanzu ya MeTL kilichopo Kurasini jijini Dar es Salaam. Wanaoshihudia tukio hilo ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq (kushoto), Afisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL Bw. Vijay Raghavan ( wa pili kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb) (wa tatu kushoto) pamoja na wadau wengine wa masuala ya Lishe.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wafanyakazi wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL mara baada ya kumaliza zoezi la kutembelea kampuni hiyo inayozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo mafuta ambapo amempongeza Mh. Mohammed Dewji kwa kutengeneza ajira kubwa kwa Watanzania kupitia kiwanda chake.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL wakimsikiliza Mh.Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete wakiwa kwenye picha ya pamoja na Uongozi wa Kampuni ya MeTL pamoja na wadau wa masuala ya lishe alipotembelea Kiwanda cha East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL katika Kampeni ya Uongezaji wa Virutubishi vya Vitamini A katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mkewe Mama Salma Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq, Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb), Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema kwenye picha ya pamoja na wadau wengine wa masuala ya Lishe.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb) (kushoto) mara baada ya kuhutubia wafanyakazi wa Kampuni ya East Coasts Oils and Fats Kampuni Tanzu ya MeTL. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Meck Sadiq na mdau wa masuala ya lishe.
Mkurugenzi Mkuu wa Makampuni ya MeTL Mh. Mohammed Dewji (Mb), akiagana na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumaliza ziara yake katika kiwanda cha EAST COAST OILS & FATS ambacho kampuni tanzu ya MeTL ikiwa ni mwendelezo wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Lishe bora kwa walaji kwa kuongezaji wa Virutubishi vya Vitamini A katika Vyakula vinavyozalishwa viwandani.

CCM YAWAPONGEZA VIONGOZI WA DINI


   Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi iliyokutana jana Mjini Dodoma imeipongeza serikali kwa hatua inayoendelea kuchukua katika kuchunguza chanzo cha tukio la mlipuko wa Bomu uliotokea Kanisani Jijini Arusha.
Bomu hilo lilirushwa Mei Tano mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Kanisa la Romani Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olisiti na kusababisha vifo vya watu watatu na majeruhi kadhaa.
 Akizungumza leo Jijini Dar es salaam Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE ameeleza kuwa taarifa hiyo ya serikali iliwasilishwa jana katika kikao hicho na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dokta EMMANUEL NCHIMBI .
 Kufuatia tukio hilo, Kamati Kuu imelaani na imeitaka serikali kuharakisha uchunguzi pamoja na kuongeza kasi ya uchunguzi wa suala hilo sanjari na kutafuta mzizi wa matukio hayo pamoja na kutoa taarifa mara kwa mara kuhusu maendeleo ya uchunguzi wa tukio hilo.
  Hata hivyo Kamati Kuu imewapongeza viongozi wa Madhehebu ya Dini nchini kwa kuweza kuwaelekeza waumini wao kuhusu mlipuko huo na kuweza kusimamia amani na utulivu tangu kutokea kwa tukio hilo.
 Pia Kamati Kuu imewataka viongozi wa kisiasa nchini kuliachia Jeshi la Polisi liendelee na kazi ya upelelezi wa tukio hilo.
Wakati huo huo, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi-CCM, Rais JAKAYA KIKWETE  wiki ijayo anatarajia kukutana na Wabunge wote wa CCM Mjini Dodoma katika kikao cha kazi. Kikao hicho kitakuwa ni cha siku Mbili kuanzia Mei 18 na 19 mwaka huu. Katika kikao hicho, Wabunge watatumia fursa hiyo kutoa maoni yao kuhusu utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010/2015 katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika Majimbo yao ya Uchaguzi.
  NAPE amefafanua kuwa Chama Cha Mapinduzi kimekuwa na utaratibu wa kukutana na Wabunge wa Chama hicho ili kujadili masuala yanayohusu nchi likiwemo suala la utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ambalo ndio Dira ya maendeleo ya wananchi.
Pia amesisitiza kuwa kuitishwa kwa kikao hicho hakuna uhusiano na suala la aina yoyote ya kuwawajibisha Wabunge wa CCM kinidhamu bali ni mkutano wa kawaida na wa kazi.
  Mara baada ya kikao hicho cha Wabunge wa CCM, Kamati Kuu ya CCM itakutana kwa siku Mbili Mjini Dodoma kuanzia Mei 20 hadi 21 mwaka huu.

UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) na Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya wametoa matamko makali kupinga kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa pamoja na Mkewe juu ya Raisi Kikwete.

Mwenyekiti wa Uwt  Mkoa wa Mbeya Prisila Mbwaga alisema kama Wanawake wa Chama cha Mapinduzi hawako tayari kuona matusi yanayotolewa na Mke wa Dk Slaa Josephine Shumbusho juu ya Mama Salma Kikwete kwamba anachangia kuibomoa Nchi.
 Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya Amani Kajuna alisema Umoja wa Vijana hauko tayari kufumbia macho matusi anayotukanwa Raisi Kikwete  na Dk Slaa anapokuwa akihutubia wanachama wake jukwaani.




 
UMOJA wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi(UVCCM) na Umoja wa Wanawake (UWT) wa Chama hicho Mkoa wa Mbeya wametoa matamko makali kupinga kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Dk. Wilbroad Slaa pamoja na Mkewe juu ya Raisi Kikwete.

Matamko hayo yalitolewa  na Wenyeviti hao katika Mkutano na Vyombo vya habari uliofanyika katika Ofisi za UVCCM Mkoa wa Mbeya, ambapo walisema kamwe hawawezi kufumbia macho maneno ya uzushi na uchonganishi kati ya Serikali na wananchi.
  
Akisoma tamko Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa wa Mbeya Amani Kajuna alisema Umoja wa Vijana hauko tayari kufumbia macho matusi anayotukanwa Raisi Kikwete  na Dk Slaa anapokuwa akihutubia wanachama wake jukwaani.
Alisema katika Mkutano alioufanya Mei 12, Mwaka huu Wilayani Mbozi Mkoa wa Mbeya Dk. Slaa akihutubia wananchi kuwa Raisi Kikwete ni Freemason,  Mdini, Mawaziri hawamsaidii pia ni Mafisadi na kuongeza kuwa ana ushahidi wa  Cd ambazo Raisi Kikwete akihamasisha udini na kuhusu uchinjaji.
Alisema maneno ya Dk. Slaa ni uzushi ambao unalengo la kufitinisha Watanzania na Serikali ya Chama cha Mapinduzi hususani anapofanya mikutano ya Hadhara katika Mkoa wa Mbeya ambapo aliongeza kuwa Ufisadi anaousema yeye kwa Mawaziri wa Ccm ili hali yeye mwenyewe anaongoza kwa ubadhilifu wa fedha za Wananchi.
Alitolea mfano wa ubadhilifu uliofanywa na Chadema mkoani Mbeya kuwa ni pamoja na Kitendo chaMwenyekiti wao Freemani Mbowe kuchangisha fedha Milioni Tatu kwa wananchi kwa kile alichodai zingetumika kununulia maji na matibabu wakati wa maandamano lakini hazikufanya kazi hiyo na hazijulikani zilipo.
Kajuna alisema mbali na fedha hizo kutokujulikana matumizi yake  pia Dk. Slaa alichangisha fedha zingine Shilingi Laki saba kwa ajili ya posho ya Wabunge waliofukuzwa bungeni jambo ambalo lilileta sintofahamu kwa wakazi wa Jiji la Mbeya.
Alisema ufisadi mkubwa uliopo ndani ya Chadema ambao kila Mwezi wanapata ruzuku ya takribani Milion mia Tatu lakini hawajawahi kujenga hata chumba kimoja cha Zahanati wala kutoa msaada kwa wananchi wasiojiweza lakini wao wanazidi kuwachangisha wananchi.
“ Jamani watanzania fungukeni muone huyu kiongozi wa namna gani Mlafi, Mchoyo na mchochezi  asiyependa kuona amani ya Nchi ikistawi” alisema Kajuna.
Aliongeza kuwa pamoja na Chadema kupata fedha zote hizo bado zinaishia mikononi mwa watu wachache hususani Dar Es Salaam ambapo Mikoani hawazipati na ndiyo sababu Ofisi za Chadema Mkoa wa Mbeya zilifungwa kutokana na kutolipia pango la Nyumba deni la Shilingi Laki tatu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Uwt Prisila Mbwaga alisema kama Wanawake wa Chama cha Mapinduzi hawako tayari kuona matusi yanayotolewa na Mke wa Dk Slaa Josephine Shumbusho juu ya Mama Salma Kikwete kwamba anachangia kuibomoa Nchi.
Alisema Shumbusho alinukuliwa akitoa matusi makubwa dhidi ya Mama Salma katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilayani Mbozi akisema ameshindwa kumshauri raisi kuhusu uongozi na namna ya kuongoza nchi.
Aliongeza kuwa katika matusi yake alimtuhumu Mke wa Raisi kuwa ni Mwanamke Mpumbavu anayeibomoa nchi nyumba yake kwa mikono yake Mwenyewe kama Biblia inavyosema na kwamba yeye atakuwa tayari kumshauri Dk. Slaa atakapokuwa Raisi mwaka 2015.

Kutokana na tuhuma hizo Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Mbeya wamemtaka Mke wa Dk. Slaa kuacha tabia ya kumsema vibaya Mama Salma na akiendelea hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Picha na Mbeya yetu

Mapitio ya Habari

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...